".......Watu
wakalibeba lile jeneza lililokuwa na mwili wa mwanangu huku wakipokezana baada
ya kila kitambo kidogo. Hatimaye wakafika nalo makaburini, wakaliweka jeneza
pembeni mwa kaburi lililokuwa limeshaandaliwa.Katekista aliongoza sala ya
mazishi, kisha zoezi la kumzika mwanangu likafuata.Jeneza liliingizwa kaburini
taratibu hadi likatua kwenye sakafu ya kaburi lile. Wakachota mchanga na
kuniletea ili mimi niwe wa kwanza kutupa mchanga kaburini japo kiganja kimoja.
Nikasisimuka mwili, taratibu nikachota ule mchanga nikaumimina taratibu kwenye
kaburi la mwanangu Sostenes. Jinsi nilivyozidi kumimina ule mchanga ndivyo na
machozi yalivyozidi kunitiririka na mengine kumiminika hadi ndani ya kaburi la
mwanangu. Nilipomaliza nikaondoka taratibu ili kumpisha mke wangu naye amzike
mwanaye. Haikuwa rahishi Mama salima kuchukua kiganja cha mchanga na kumimina
kwenye kaburi la mwanae, basi wanawake Fulani walimshikilia na kumsaidia hadi
akatupa mchanga ndani ya kaburi la mwanae. Akafuata Sabrina japo naye kwa kushikiliwa.
Ndugu wengine wakafuata na baadaye wengine wakalishambulia kaburi la mwanangu
kwa kutupia mchanga kwa kutumia spedi na kushindilia kwa visigino vyao. Mimi
nikiwa nimesimama pembeni niliwaza moyoni mwangu, nikajaribu kukumbuka
mwanangu, machozi yakaanza kutoka tena. Kaburi lilipojaa wakaanza kushindilia
kwa mikono. Mama Salma, mama wa marehemu alilia kwa nguvu hadi nikamwonea
huruma japo mimi mwenyewe nilishikwa na uchungu sana kumpoteza mwanangu.
Kisha
tukaweka mataji kwenye kaburi la mwanangu, nilianza mimi akafata mama yake
akafuata Sabrina dada yake na kisha wajomba, binamu, shangazi na ndugu wengine
wakafuata. Mazishi yalipomalizika mtangazaji, mzee Ndeluvale akatangaza kuwa
watu warudi nyumbani kwa wafiwa wakanawe mikono, akimaanisha wakale chakula.
Basi watu wakaanza kurudi, mimi nilikawia kidogo, nilitamani kama nibaki
kaburini lakini ilinilazimu niondoke.
Tulipofika
nyumbani chakula kilikuwa kimeandaliwa, watu wakala wakashiba na kusaza. Mimi
sikuweza kula mchana ule. Nilianza kufatilia kujua hali ya binti yangu Salma
aliyekuwa amepoteza fahamu wakati wa kwenda kuaga maiti ya mdogo wake. Hali ya
binti yangu ilikuwa shwari, nikatiwa matumaini.
Usiku
watu waliobaki kukesha na kuomboleza pamoja nasi, walikuwa wakiimba nyimbo za
aina nyingi. Baadhi ya nyimbo hizo nilikuwa nazifahamu na nyingine zilikuwa
ngeni kabisa kwangu. Nyimbo nilizokuwa nazifahamu ni kama vile ule unaoitwa
Twiwalala:
Uliimbwa
hivi:
Moooja,
mbili tatu twende twiwalala, (We twiwalala) x 2
Ve
twiwalala umwanavesu(We twiwalala)
Umwana
vesu asivoneha (We twiwalala)
Umwana
vesu ahele hwina (We twiwalala)
Moooja,
mbili tatu twende twiwalala, (We twiwalala) x 2
Pia
waliimba ule wimbo wa“Parapanda italia,” pia na nyimbo nyingine nyingi
zilizomtaja na marehemu mwanangu. Tulifarijika kwani watu waliguswa na kifo cha
mwanetu hata wakashiriki nasi katika tukio hilo. Uliipoimbwa wimbo
wa`twiwalala` sikusita kusimama na mimi kuimba. Kwa kawaida wimbo huu
unapoimbwa kwenye msiba watu huanza kucheza kwa kuruka na kuzungukazunguka
wakipapasapasa kama vile wanatafuta kitu kilichopotea na kwa wakati ule hakika
ulikuwa ni wakati wa kumtafuta mwanangu Sostenes. Hivyo nilijumuika nao
kupapasa kumtafuta mwanangu.
Tulicheza
tukaruka tukiimba huku tukipiga yowe, huuuuwi, huuuuwi! Mara tukaanza kuondoka kuelekea
makaburini. Akina mama fulani waliokuwa wanaimbisha walitangulia mbele, mimi
nilikuwa katikati ya watu wengine, nami nilikuwa nikiimba kwa sauti kwani wimbo
ule nilikuwa naufahamu vizuri na nilikuwa naupenda. Tukashuka ule mteremko mara
tukakata kona, tukapitiliza vile vichaka vilivyo jirani na makaburi hatimaye
tukaingia eneo la makaburini usiku ule huku tukiimba kwa sauti na kupiga yowe.
Hapo sasa na mimi nikaharakisha nikawa mbele jirani na wale akina mama
waliokuwa wanaimbisha. Kwa mbali niliweza kuona eneo ambalo tulimzika mwanangu.
Tulivyozidi kusogea kwa mbali niliona kama kitu cheusi mfano wa kifurushi
kikitoweka kutoka pale lilipo kaburi la mwanangu. Nilishituka ghafla nywele
zikasimama, mapigo ya moyo yalienda kwa kasi, moyo ukadunda duf-duf-duf kijasho
chembamba kikaanza kunitoka.
__________inaendelea_______
RIWAYA: KUMBE JIRANI YANGU MCHAWI
MTUNZI: ELIAS K. MWALONGO
SIMU: +255769313224
E-MAIL: mwalongoelias7@gmail.com
~~~MPENDWA
MSOMAJI~~~
Nendelea
kukuonjesha tu vipande vya Riwaya hii maridadi. Kitabu cha Riwaya hii ya
kusisimua kinapatikana kwa tsh. 5000/-Tu.
Lakini
pia KANTON PRINTING inakukaribisha kuwa dalali wa KITABU hiki popote ulipo
ndani ya Tanzania, endapo uko tayari basi, utauziwa vitabu vya jumla kwa Tsh.
2500/-kila kimoja nawe utaenda kuuza kwa tsh.5000/-kama ilivyokwishaonyeshwa
kwenye kitabu hicho. Endapo utakuwa tayari kuwa dalali basi itakupasa kuchukua
walau kuanzia vitabu 20 na kuendelea. Ambapo vitabu 20 utachukua kwa
tsh.50,000/- wewe utaenda kuuza kwa tsh.5000/-kila kimoja na kupata
sh.100,000/-
Kwa
maelezo zaidi wasiliana na mtunzi wa Riwaya hii No. +255769313224
Asante
na Ubarikiwe mno!
