Thursday, 14 December 2017

NITAKUPENDA DAIMA


Mtunzi: Elias Kalistus Mwalongo
Chuo Kikuu Cha Kikatoliki Ruaha(RUCU)
Simu: 0769313224
____________
Laazizi wangu wa moyo, natamani nikunong`oneze maneno matamu lakini najikuta niko hoi tena hoi kabisa, nashindwa nianzeje. Umebarikiwa kati ya waliobarikiwa na umetunukiwa vyote vigezo.
Hakika nimekuchagua wewe kati ya waliotunukiwa sifa na vigezo lakini umewazidi mbali mno. Nikikutazama sura yako wala siwezi kukumaliza leo wala kesho kutwa. Kidevu kilichochongoka, pua ya saizi halali, shingo kama ya kangaroo na macho ya yalolegea yenye kukonyeza haki ya nani umeniteka nimekubali tu niwe mateka wako.
Ole wangu sasa nione kifua chako chenye mwinuko, mgongo tumbo na kiuno chenye saizi ile ninayoipenda mimi, mashallah, nahisi labda ni mmakonde fulani kanichongea vile ninavotaka, kumbe la hasha ni mwenyezi mwenyewe kakuumba kwa ustadi mkubwa hivyo.
Nyuma sasa sigeuki na mbele ni siri yangu, lakini mguu wa saizi wenye mvuto, kucha, vidole, mabega na mikono, nimefumbwa macho sioni kasoro yoyote kwako, amaa hakika mwenyezi ashukuriwe kwa uumbaji.
Nywele zako kichwani uziseti vile ninavopenda, halafu masikio utundike na heleni nzuri zinazongaa uziache tu zinaning`inia kama bangili, walahi sikuachi, naomba uniteke zaidi, ongeza na walinzi ili nisitoroke.
Ili nikome kubwabwaja maneno, naomba sogea mpenzi wangu unikumbatie kumbatio la mahaba, nijilaze kifuani pako huku nikideka kwa deko nawe unidekeze nidekezeke nisahau shida zote za hapa duniani hata nijisikie niko paradiso najivinjari.
Nikumbate unipetipeti vyovyote vile maana nishakuwa hoi taabani, akili yangu yote imehamia kwako sikumbuki kingine chochote. Nikikuangalia usoni muda mwingine nahisi labda ni malaika fulani kanitembelea kumbe ni wewe laazizi wangu wa moyo ambaye nimekuchagua mwenyewe. Umesheheni sifa nyingi nami nimekusujudu sina kwa kwenda kwingine maana kwako ndio nimefika, nimetua mabegi na vilago vyangu.
Tena sitavuta subira, nitakupeleka ndani uwe mama wa wanangu na mimi ndio baba. Walimwengu watabaki kutushangaa lakini ukweli utabaki hivyo hivyo. Maneno yao wakiongea wala usijali maana huwa hawaishiwi ya kusema. Najua tu kuwa ya kwao watayatia mfuniko na yangu watayachezea mdundiko, wala usiwazingatie.
Nakupenda wewe tu laazizi wangu, wengine watabaki kuwa wifi zako. Naapa kuwa NITAKUPENDA DAIMA ili nihakikishe kuwa sikupotezi kwa uzembe.
Naomba usichoke kunipenda, kamoyo kangu kadogo nimekaegesha kwako kote, naomba ukatunze kasipate majeraha, nisije nikajifia mwenzio.
Laazizi wangu wa moyo, nitakupenda daima!
Ahsante sana! 
_

1 comment:

  1. Baada ya kuwa na uhusiano naye kwa miaka saba, aliachana nami. Nilijaribu kila niwezalo kumrudisha lakini yote yalikuwa bure. Nilitamani arudi vibaya sana kutokana na mapenzi niliyonayo kwake na nilimsihi kwa moyo wangu wote, nilimpa ahadi lakini alikataa. Niliwasiliana na mganga aitwaye DR Dawn, ambaye angeweza kunisaidia kuniroga ili kumrejesha lakini mimi ni mtu ambaye sikuwahi kuamini uchawi, sikuwa na jinsi zaidi ya kujaribu. Nilimtumia barua pepe mganga huyo na akaniambia kwamba hakuna tatizo lolote, kwamba kila kitu kitakuwa sawa baada ya siku mbili na kwamba mpenzi wangu wa zamani angerudi kwangu baada ya siku tatu. Alipiga uchawi na cha kushangaza, siku ya pili, ilikuwa karibu 4:00 PM. Mpenzi wangu wa zamani alinipigia simu, tukasuluhisha tofauti zetu na sasa tuna furaha pamoja. Yeyote anayeweza kuhitaji usaidizi wa mtangazaji huyo anaweza kumtumia barua pepe kwa ( dawnacuna314@gmail.com ) au /WhatsApp kwa: +2349046229159

    Kwa uchawi wa kuungana tena.
    Kwa ujanja wa ujauzito.
    Kushinda bahati nasibu.
    Kushinda kesi mahakamani.
    Mimea ya kutibu, kila aina ya magonjwa kama,
    VVU UKIMWI Kansa malengelenge na zaidi.

    ReplyDelete

NITAKUPENDA DAIMA

Mtunzi: Elias Kalistus Mwalongo Chuo Kikuu Cha Kikatoliki Ruaha(RUCU) Simu: 0769313224 ____________ Laazizi wangu wa moyo, nat...