Thursday, 16 March 2017

BINTI YAKO AMEROGWA



BINTI YAKO AMEROGWA



Mtunzi: Elias K. Mwalongo (Kanton)
Ruaha Catholic University (RUCU)
Simu: +25576933224 Tar. : 09/03/2017

 ```````````````````````````````````````````````````
Jamani mama Atu, ivi kwani umesahau siku ile ulipojifungua, ukamzaa binti yako ulivyo furahi? Sisi majirani zako tulipopata habari zako hatukubaki nyuma. Tukaja mbio mbio tukupe mkono wa `hongera` kwa kuwa umeanza kuitwa Mama. Tulijua mkono mtupu haulambwi, basi tukajibebesha, pakiti za sukari ya mtoto, pakiti za chumvi, vifurushi vya unga, na vifurushi vingi tele tukatua kwako, tukakwambia “hongera wifi yetu, umekuwa mama sasa”. Hatukuwa na shaka sisi juu ya malezi yako kwa mwanao. Tangu angali mdogo tulikusihi umlee vizuri mwanao naye atakuja kukulea umri utakapokuelemea. Hongera kwa juhudi zako. Tulikushuhudia, ukithubutu hata kumchapa bakora alipokuwa akikosea, ndio malezi. Ulimfundisha mengi kwa kweli. Ulimtuma sehemu alienda mara na kurudi kwa wakati. Akikutana na ndugu au watu waliomzidi umri, ulimfundisha awasalimu kwa adabu. Asante sana, tulijinoma `shikamoo` zake. Alikuwa mtoto mzuri, mtulivu, mwenye heshima na staha. Hakika fahari ulijinyakulia Mama Atu, maana jema alitendalo mtoto ni fahari kwa mzazi.
Shule umempeleka kama kawaida, tena shule za maana, sio za kubabaisha. Kwa tabia yake matokeo yake pia yalikuwa mazuri, sifa zake tulizisikia kwa wanetu maana mwanao alikuwa kiboko yao darasani. Fahari ilioje Mama Atu uliifaidi. Mwanao akafahamika shuleni na hata mtaani huku, kwa tabia njema na ufaulu mzuri darasani. Heko sana mama Atu kwa malezi uliyompa mwanao. Kidato hicho kikaisha, akaingia cha pili, hali akizidi kuwatupilia mbali wenzake kwenye mitihani. Tusio na kinyongo wala roho mbaya tulikwambia “hongera Mama Atu”, kisha tukamgeukia binti yako Atu, pato lako mashuhuri la ujanani tukamwambia, “Kazana mwanetu”. Kidato cha tatu akaingia huku matumaini yetu kwake yakibaki kuwa makubwa. Mhula wa kwanza sifa zake za tabia ziliendelea kuvuma hapa mtaani kwetu, japo mwishoni mwa mhula katika mtihani wake hakuwa wa kwanza tena, maana alipitwa na Tekla binti wa Shomeho, huku Daniel yule mtoto wa Mtotofu akiwaongozea, kwa kushika namba wani. Tulidhani wamekosea kusahihisha au wamekosea kujumlisha alama au labda wamechanganya alama hizo lakini wala, hizo zilikuwa alama zake mpya zilizo halali. Tulibaki mdomo wazi kumshangaa binti yako, anakoelekea kimasomo.
Kama kawaida yetu sisi, halilali jambo, taarifa tukazipata nasi tukazileta kwako na kuzitua kama zilivyo. Wengine wakatwambia, binti yako hata tabia imebadirika. Tulipoduwaa ndo wakapigilia zaidi, mara wakasema binti yako ana kiburi, mara wengine wakasema, Atu, anadharau, mara wakasema anamajivuno. Tukabaki kuwa wasikilizaji. Wakatuvunja ukimya walipotwambia eti binti yako anajihusisha kimapenzi na mwanafunzi mwenzake wa kidato cha nne na kijana mmoja fundi ujenzi hapa kijijini. Masalale! Kauli ilitutisha tukajua Atu atapotea. Kwa kihelehele chetu tukafunga kanga kiunoni tukaja mbio tukusihi UMKANYE MWANAO. Tukarudi tumelowa matusi. Ulitutusi tulipokusihi umkanye mwanao maana anakoelekea kubaya. Ulituzodoa, ukatubinulia midomo usitake kuzingatia ushauri wetu. Tuliambiwa tukaja kukwambia, ukatutusi, hata matusi ya nguoni ili tukome kabisa kukufatilia. Mama Atu, tunakumbuka yale matusi yako eti, “mtakwisha kuni zenu kwa kutupikia machegea, na hatutalia gizani kwa kuwaogopa majirani. Yenu mwayatia mfuniko yangu mwayachezea mdundiko. Hakika, Mola nipe radhi mie kuishi na watu kazi….” Haya Mama Atu!. Uliona kuishi na sisi kazi, tulipokuasa uliona tunakufatilia, haya sasa binti yako hatamaniki.
Binti yako uliyejivunia sasa AMEROGWA. Ulimfundisha kusalimia, sahizi hatuambulii salamu yoyote toka kwake. Tukimuita japo kwa nia njema, anatubinulia midomo. Wageni tukifika kwako, binti yako anatudharau. Yeye nyumbani hakukaliki, anashinda anazurula wapi, sisi hatujui. Halafu, jamani Mama Atu, na hizo nguo ambazo mwanao anavaa mbele za watu unamnunulia wewe mwenyewe? Anatulia aibu sisi wazazi wake. Sura yake masikini, kwani pale zamani alikuwa mweupe hivi au amejichubua? Jamani, ivi ni Atu yuleyule tuliyemletea, pakiti za sukari siku ile? Ndiye yule tuliyekuja kumsalimu kwa furaha na bashasha tukampakata mikononi mwetu nasi tukajisikia fahari? Ni yule yule Atu alikuwa akiongoza mitihani darasani na kuwapita wanetu? Ndiye Atu yule aliyevuma kwa sifa kemkem hapa mtaani?. Halafu naomba kuuliza, kama ni unoko wacha niwe mnoko tu, Atu alikuwa akisoma darasa moja na binti yangu Faraja, binti yangu alipitwa na Atu kila mtihani maskini, na sikutaka hata kulinganisha, nilimchukulia mwanangu kama kilaza ukimlinganisha na wako. Lakini eti, Atu ana cheti cha kidato cha nne? Ana cheti cha kidato cha sita? Au kote huko mbali mno, mtihani wa kidato cha nne alifanya?? Kulikoni Mama Atu?? Binti yangu Faraja, alihitimu hadi kidato cha sita, na sasa na chakarika kukusanya visenti binti yangu amalize chuo. Isitoshe hata mkopo amekosa, lakini kwa namna yoyote ile atasoma, hata bagia nitatembeza, nipate chochote mwanangu asome. Tabia yake bado inaridhisha, namtegemea atakuja kunisaidia umri utakaponielemea. Mama Atu mimi nilimkanya alipoonesha kubadili tabia na kufata mikumbo, nilikaa naye na kumuelimisha mengi juu ya maisha haya. Wewe ulikaidi, ulisahau kuwa anaweza kubadirika. Dunia imemroga, Utandawazi umemroga, Digitali imemroga, Makundi mabaya yamemroga. Sasa yuko hapo alipo, amechoka hatamaniki, japo umri wake bado mdogo lakini anapakata mtoto wake mchanga, ambaye sisi hadi leo hatujui baba yake ni nani. Mdharau mwiba mguu huota tende, endelea kumlea binti yako, mlee pia na mjukuu wako maana hakuna namna. Tulipokuasa tulikuwa na nia njema na sio kukufatilia. Kila mmoja anavuna alichokipanda Mama Atu. Tukutakie kila la kheri na maisha mema.
 ___________________________
KWA MAONI NA USHAURI, WASILIANA NA MTUNZI WA TUNGO HIZI ELIAS MWALONGO - 0769313224

Wednesday, 8 March 2017

HOW I TOOK YOUR GIRLFRIEND-Elias Mwalongo



HOW I TOOK YOUR GIRLFRIEND
BY: Elias K. Mwalongo(Kanton)

Ruaha Catholic University(RUCU)

Cont. 0769313224
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
        



        The first day I met your girlfriend,

I was so invited to talk to her,

I simply started with hi dada!,

She smiled and replied hi kaka!.



My smile was enough to make her mine,

Her reply penetrated into my heart,

The more we went on talking,

The more she was sticking to my heart.



I asked for her phone number,

I smiled a little when she gave me,

My heart happily said “it`s over!”

Hence I had to prove that its real over.



I called her and sent texts every moment,

I tried to be close to her, I managed!

I did not care that she was yours,

I said `potelea mbali` I must win!



Day to day I made her important,

I leant what she prefers most in life,

I knew also what she hates most,

Slowly she seemed to give me priority



I wrote romantic poems to her,

I gave her my time and attention,

I never made her cry but only smile,

I gave her everything she asked for.



I gave her my heart, I took care of her,

I was a reason for her joy and smile,

I gave what she wanted, I gave her my life,

I made her very important person to me.



Several times she came home to meet me,

I also went to visit her at their home,

I desired to be with her all the time,

I loved he very much, she loved me too.



When you left her to cry, I cried with her,

You did not text her, I sent her a poem daily,

I gave her my time, you pretended to be busy,

As you ignored her, I made her very important.



Dear brother, the Ex-boyfriend of Sabrina,

This is how I simply took your girlfriend,

I love her, I know how to handle her carefully,

We love one another, thanks to God!

~~~~~~~~~~Done~~~~~~~~~~
“Call me for more Romantic Poems”

NITAKUPENDA DAIMA

Mtunzi: Elias Kalistus Mwalongo Chuo Kikuu Cha Kikatoliki Ruaha(RUCU) Simu: 0769313224 ____________ Laazizi wangu wa moyo, nat...