OLE WAKO MIMI NIFUKUZWE SHULE
NITAKUFA NA MTU
Na: Elias K. Mwalongo(Kanton)
MAOMBOLEZO
YA MTOTO MCHANGA TOKA KABURINI KUMLILIA MUNGU!
|
I
|
likuwa
siku ya Jumamosi fulani (Weekend) Anton (ambaye baadaye atakuwa
baba yangu) na Anna (ambaye baadaye atakuwa mama yangu), baada ya mlo wa mchana
walitoka hapo shuleni X na
kuongozana katika matembezi yao. Baadaye walifika BANDA-BEACH. Baba Anton
alitaka kumsadikisha Anna kuwa yeye ni Kizito, alimnywesha ile mbaya akalewa
hadi chakaraa. Walipoamua kurudi shuleni, giza nene lilikuwa limeshaingia. Wote
wawili wamelewa hoi kabisa. Sasa hata tamaa zao za mwili ziliwatawala.
HAWATUONI `Ee; Mungu niende
umbali gani Ili nijifiche mbali nawe? Nikisema nipande juu sana Mbinguni, huko ndiko uliko Ee Mungu. Nikitwaa
mbawa za asubuhi ili nifike Mashariki ya mbali, hata huko mkono wako wenye
nguvu utanifikia Ee Bwana. Nikijificha katika giza nene,giza nalo ni sawa na
mchana mbele yako Ee Bwana. Basi niende wapi au nijifiche wapi ambapo Mungu
hayupo ili niweze kutenda uovu huo? Sote hapa duniani ni kama sisimizi tu
mkononi mwako Ee Bwana, kwa sababu Enzi yako ni kuu mno;Ni nani aliyepima maji
yote ya Ulimwengu kwa konzi ya mkono wake?(Isa;40:12ff)Na kuzikadiria Mbingu
kwa shubiri,na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi,na kupima milima na
vilima kwa mzanii?Ni nani aliye mfundisha Mungu njia ya hukumu,na kumfunza maarifa
na kumwonyesha njia ya fahamu? Tazama mataifa ni kama tone la maji katika ndoo,
huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama,si kitu mbele zake, huhesabiwa kwake
kuwa duni na si kitu ni ubatili. Basi mtamlinganisha Mungu na nani? Au mtamfananisha
na mfano wa namna gani? Je, hamkujua toka mwanzo kuwa yeye ndiye azitandazaye
Mbingu kama pazia, na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa,ndiye awatanguliaye
wakuu na kuwabadilisha hao waamuzi wa dunia!.`
ΓΌ MATOKEO YA ULEVI ULE
Siku ile Baba yangu Anton na Mama yangu Anna
walivunja sheria ya shule kwa kutofika shuleni kwa rollcall. Siku ile walipoteza hela katika ulevi na uzinifu, siku
ile waliharibu afya zao za roho na za mwili, siku ile walipoteza heshima yao
kwao wenyewe na kwa watu waliowaona, siku ile walijitenga na Mungu kwa ulevi na
uzinzi, siku ile walirudi shuleni maskini na maskini zaidi kiroho, siku ile
walimleta mtoto (mimi) duniani watakayemwua baadaye. Siku ile walibaini kuwa
Elimu walioipata haikuwasaidia kitu, Imani/dini yao bado haikuwakomboa, wala
mazingira hayakuwakomboa na hawakuwa na nidhamu. Pia siku ile nililetwa duniani
na wazazi kutokana na ulevi wao tu.
JANUARI 5; Uzima wangu umeanza leo. Ndio siku ile
waliyokutana wazazi wangu pale kichakani kwa sababu ya ulevi wao. Lakini wao
mpaka sasa hawajagundua mwanzo wa kuishi kwangu. Ningali mdogo sana hivi wala
sionekani kwa macho matupu ila kwa darubini kali ninaonekana kama kichwa cha
sindano. Lakini hata hivyo tayari mimi ni mtu
kamili niliye nafsi yangu kabisa. Mambo yangu yote yamejisuka kabisa.
Maumbile yangu na tabia yangu tayari inaeleweka, Mfano; Macho yangu yanafanana
na ya mama yangu, na nywele zangu zinafanana na zile za Baba yangu, za mviringo
na nyeusi.Tazama tayari imeshadhihirika kuwa nitakuwa mvulana. Na Mungu tayari
anataka niwe Padre wa kuzipeleka Roho za watu tele kwake.
JANUARI 19; Sasa mishipa yangu ingawa ni midogo sana, imeanza kukua
na chembe za damu yangu zinaendelea kutengenezwa haraka sana. Bila shaka sasa
hivi hakuna hata kiungo kimoja kilichokamilika. Kumbe, bado nategemea damu ya
mama yangu inayoniwezesha kuendelea kuishi hadi sasa, kama chakula changu, bado
nitamtegemea sana yeye hata baada ya kuzaliwa kwangu, maana ndicho pekee
chakula changu bora.
JANUARI 23; Sasa hata midomo yangu imeshakua, kutosha kuweza
kuifungua. Baada ya miezi 12 tu au hata pungufu, nitakuwa nikitumia midomo hii
kuwasalimu wazazi wangu kwa tabasamu na kwa gugumio la furaha tele na neno la
kwanza kulitamka litakuwa “MAMA” Je,
Mama yangu hatafurahi kusikia sauti hii nyororo ya mtoto wake!?
JANUARI 25; Hata moyo wangu sasa umeanza kupigapiga. Na utaendelea
kudundadunda daima hadi mwisho wa maisha yangu. Je! Unaonaje? Hii si ajabu na
ya kupendeza kwa wote wenye mapenzi mema?
FEBRUARI 2; Kumbe sasa hata mikono na miguu yangu imeanza kukua.
Ndiyo, nafahamu kuwa bado itanichukua muda mrefu ili kuitumia vema baada ya
kuzaliwa kwangu. Haidhuru, nitavumilia bado!
FEBRUARI 12; Kumbe sasa hata vidole vyangu vya mikononi vimeanza
kukua. Hii ni ajabu sana, kwa sababu, mikono yangu hii itashikana na watu wote
nitakaokutana nao. Na mikono hii itaweza kujifanyia marafiki tele, kwa
kusalimiana na kushikana nao. Kujifanyia kazi yangu mwenyewe, kama vile kusali
Misa Takatifu, kugawa Komunyo Takatifu, kuungamisha, kubatiza watu, kupaka watu
mafuta matakatifu n.k.
FEBRUARI 20; Tangu siku ile Mama yangu
amegundua kuwa hakwenda hedhi/mwezi, halafu alijisikia kutapika, ukinaifu,
kukosa hamu ya chakula, maumivu na uvimbe kidogo wa matiti yake, leo aliamua
kwenda kumwona mganga.Naye mganga maskini wa unyofu wake wote, alimhakikishia
kuwa asiwe na shaka yoyote,mimi nilikuwa nimetungika mimba na ni mzima kabisa
na nipo njiani mwa kuzaliwa.
`Oh!Oh!!!`
Alitamka Mama yangu. Hizi zilikuwa ni habari mbaya kabisa, zilizomtoa roho mama
yangu hata kuchanganyikiwa akili na kukonda rohoni. Alipiga masumbwi (ngumi)
tumbo lake ili kuniua kama ingewezekana. Alilia machozi kumtiririka machoni na
kujenga chuki sana juu yangu na hata juu ya Baba yangu Anton, kwa sababu
nimetungika mimba. Hakuamini maneno ya mganga.
Siku ileile, alienda mbio na kwa hasira sana kwa baba yangu Anton. Salamu ya
kwanza aliyoweza kutoa kwa Baba yangu Anton aliyekuwa chumbani kwake, Bweni la
wavulana alisema, “Ninamimba yako Anton, Ole wako nikifukuzwa shule”, Baba
yangu Anton nilimwona kama aliyechanganyikiwa akili. Alikunja ndita, macho yalimwiva na kamasi kumtoka ovyoovyo
tu, aliondoka mle chumbani akatawanyika zake porini.
FEBRURI 25; Mimi bila kujua hili
wala lile analowaza Mama yangu. Nilitamani watu wawambie wazazi wangu
kuwa Mimi ni mvulana. Hivi tangu sasa wangeweza kuanza kufikiria jina kwaajili
yangu. Lakini kadiri siku zilivyoendelea mbele nilonja sipati tena upendo wa
mama yangu bali chuki na ubaridi. Nilianza kuonja upweke kabisa. Laiti
ningalijua yanayoningojea masikini!!!!.
FEBRUARI 28; Sasa viungo vyangu vyote
vimekuwa vikumbwa, vimekamilika tayari, vyororo na vinapendeza hata kuvitazama.
MACHI 10; Nywele zangu tayari ni nyeusi sana, na macho yangu ya kikahawia (brown)
yameanza kukua. Je!Mama yangu sasa hata furahi kuona macho yangu yanafanana
sana na yake? Na nywele zangu za mviringo zinafanana na za baba yangu? Hata
mimi mara baada ya kupata fahamu nimejiandaa kutoa tabasamu kubwa sana pale
nikapoziona mara ya kwanza sura za wazazi wangu wapenzi.
MACHI 13; Bado kitambo kidogo sana sasa hivi karibu nitaweza kutazama mimi mwenyewe
kwa macho yangu. Bado kuna ubapa mwembamba tu unaonizuia nisifungue macho
yangu. Natamani daima na kungojea kwa hamu kubwa macho yangu yataona nini na
rangi ya vitu vya dunia hii. Lakini kuliko yote, furaha yangu kubwa sana
itakuwa hasa kuwaona wazazi wangu. Kwanini sasa inachelewa kufika upesi?
Mama yangu wee! kumbe kuna bado miezi mingine sita ya
kungoja!! Lakini haidhuru nitavumilia bado vilevile!
MACHI 24; Tazama, hata moyo wangu
sasa umekamilika. Tena hauna dosari yoyote. Ahsante Mungu, moyo wangu ni salama salimini. Sasa
nafurahi nitakuwa mtu mwenye afya nzuri. Nitayafurahia maisha yangu kwa
kujifanyia kazi zangu mwenyewe.
MACHI 28; AAAHHH!!! Mungu wangu
weee! Leo Mama yangu Anna, ameniua maskini mimi, jamani.
Tangu siku ile alipomwendea yule mganga naye
alipomwambia kuwa nilikuwa nimetungika mimba, amekuwa akikutana na Baba yangu
mara nyingi sana, nao kila mara walijadiliana mengi ya ugomvi, matusi, chuki na
kero nyingi kati yao. Kila mmoja anamnyoshea kidole cha hasira mwenzake na kusema, “OLE WAKO MIMI
NIFUKUZWE SHULE,NITAKUFA NA MTU”
Neno la mwisho nililoweza kulisikia toka kwa baba yangu ni
hili, “Wee binti, ambaa upesi na
tawanyika hapa, usinijue mimi tangu leo wala kunibughudhi, wala usinifanyie
uchuro. Ondoka kwangu we Fisi jike na kongwe. Aliyekwambia hiyo mimba ni ya
kwangu nani? Mimi kwanza sikujui kabisa! Umekuwa kiruka njia kwa kila mvulana
hapa shuleni na sasa unataka kunitupia mimba zao mimi? Eboo! pole sana binti!
imekula kwako hiyo!”.
Hapo mama yangu alitoka
anapepesuka kama amelewa, ananawa machozi usoni huku akijisemea peke yake,
“Sitaki sitaki, hata mimi sitaki hili toto lako. Loo! nifukuzwe shule kwaajili
yako! Hapana hapana! Mtoto(mimi) nitamtunzaje na shule nikifukuzwa na bila
shaka sote tutafukuzwa. Na wazazi wangu bado hawajui. Wakijua nitaingia nyumba
ya nani?”
Basi
niliona mama yangu anarudi kwa yule mganga na kuomba aitoe ile mimba yaani
aniue mimi. Mganga alidai za mchuzi.
Hapo niliona mama yangu anafungua pochi yake na kuchomoa noti chache na kumpa
yule mganga. Naye alizipokea haraka na kuweka mfukoni. Hapo sasa hata mimi
nilianza kuona damu yangu inanuka mdomoni mwangu. Yule mganga alichukua dawa
fulani, niliweza kusoma jina la dawa ile, chupa yake ilikuwa imeandikwa `Salt Poisoning` Akaitia ile dawa katika sindano, naye
akaichomeka ile sindano katika mwili wa mama yangu na kuiminya ile sindano,
nayo dawa ikaanza kusogelea kitovuni pangu polepole. Kama ujuavyo kile kitovu
ndio njia yangu maalumu ya kupatia chakula changu toka kwa mama yangu.
Aaaah!
Dawa ile!! Dawa ile jamani!! Kweli kabisa dawa ile! Bado toka kaburini
ninaikumbuka sana dawa ile `salt Poisoning`. Ilishuka polepole tumboni
mwa mama yangu kadiri yule mganga alivyoiminya ile sindano, ilishuka kama kisu
kikali sana kinachonisogelea kutaka kunichinja na kunichanachana kama vipande vya nyama ya kuchoma mshikaki.
Hatimaye iliingia kitovuni pangu na kupenya mwili wangu mzima kwa njia ya damu
yangu. Jamani! Jamani! mmh, kwanini lakini mama kuniua?
Mara
nilianza kupiga chafya, kutaka kulia nikashindwa, kukimbia pia nisiweze, kusema
nako nikashindwa. Mwili wote ulikuwa wa moto kabisa. Viungo vyangu vyororo
vilianza mara kuchanika na kunyong`onyea vyote kabisa. Mifupa yangu ikaanza
kusagika kama mchanga na mwili wangu kuyeuka kama nta ya mshumaa na kuwa kama
uji.
Jamani! Jamani! Mnionee huruma mwenzenu.
Niliwatazama kwa huruma yule mganga na mama yangu wanavyonichakaza maskini
mimi, mtoto wa mtu. Nilivuruguta na kusononeka na kumtazama mama yangu kwa
macho ya huruma na maombolezo, lakini alikunja uso wake kabisa na
hakunijali,nami nisimwone mtu wa kunisaidia.
Mara
mikono yangu ilitupwa huku na miguu kule, tumbo huko, kichwa changu huko na
matumbo yangu yakakunjuka kama kamba. Macho yangu yalinitoka nje pima.
Ndipo nilipotoa pumzi yangu ya
mwisho masikini, kuitoa roho yangu yenye huzuni na majonzi tele na mkato wa
tamaa wa kuishi tena hapa duniani. Jamani! Kweli watu wema hawana maisha marefu
hapa duniani!
NDIPO PAMOJA NA AYUBU NA NABII YEREMIA NILIPOFUNUA KINYWA CHANGU NA KUILANI SIKU NIKIYOTUNGIKA MIMBA!!
Baada ya hayo yote kunisibu,
ndipo nilipofunua kinywa changu nakuilaani siku ile yangu ya mkasa, nikisema “Na ipotelee mbali
ile siku niliyotungika mimba mimi. Isibarikiwe siku ile niliyotungika mimba na
wazazi wangu.
Siku ile na iwe giza daima. Siku ile na Mungu asiiangalie toka mbinguni.
Siku ile wala mwanga wa jua usiiangazie. Ishikwe na giza tupu, wingu na
litandwe juu yake. Tena usiku huo, na
ushikwe na giza kuu, usihesabike katika siku za miaka, wala
kutiwa hesabu ya miezi. Nawalaani hao walaanio mchana. Tazama usiku huo daima
uwe tasa wala ndani yake msiwe na sauti ya shangwe. Siku hiyo sitaisahau
maishani mwangu. Sasa nafahamu vizuri sana kwanini saa ile Yesu alilia pale juu
ya msalaba, “Mungu wangu! Mungu wangu! Mbona umeniacha? Nami siku ile nililia
kwa huzuni kali “Mama yangu! mama yangu!
Mbona unaniua? Jamani! Kifo ni kichungu, si cha kuombea kikufike, omba
jingine.
ΓΌ KILIO CHANGU TOKEA KABURINI
Toka kaburini naendelea kujiuliza, wala jibu toka
kwa Mama yangu sipati wala toka kwa watu wengine sipati.
Baada
ya mganga kuingiza koleo tumboni kwa mama yangu alianza sasa kunyofoa na kutupa
nje mifupa yangu yote na nyama ya mwili wangu akatumbukiza kwenye lindoo fulani
bovu! Halafu mganga akamwambia Mama yangu, haya sasa tayari, toa nje na kutupa
jalalani au fukia. Mama yangu aliichukua ile ndoo mbovu, yenye vipande vya
mwili wangu akaendanayo porini kidogo, akachimba pale shimo dogo, hapo akamwaga
mwili wangu akaufukia.
Jamani kilio changu mwenzenu
kinatoka bado pale udongoni aliponifukia Mama yangu mpenzi. Pale mpaka sasa
bado mwili wangu unapumzika kungojea
hukumu yangu siku ya kiama.
Enyi mnaopita karibu na kaburi langu, naomba
kujiuliza kwenu wenzangu nifahamu; Mliwatendea nini mama zenu mlipokuwa kama
mimi hata wakawahurumia wasiwaue? Mbona hamkuweza kusema kama mimi, kulia kama
mimi, kujitetea kama mimi? Au mliwafurahishaje mama zenu, mbona mwenzenu leo
nauawa na mama yangu tangu tumboni mwake? Nanyi wenzangu mliouawa na kutupwa
chooni au porini kama mimi, njooni tumlilie Mungu, kilio chetu cha maombolezo.
Abel alimkosea nini Kaini? Watoto mashahidi waliochinjwa bure na Herode wakati
wa Yesu walikosa nini? Kosa langu hasa lilikuwa ni nini? Jamani mimi
sikuwachagua wazazi, sikuwalazimisha wanilete duniani, wala sikuwaomba siku ile
wakutane pale kichakani. Mama yangu mpenzi, mimi nilikukosea nini?Tabasamu na
pendo langu kwako nilivyoviandaa kukutolea mara baada ya kuzaliwa kwangu, nawe
kwa hili unalilipa kwa kifo cha uchungu namna hii Mama!! Ulikubali ile dawa
inisagesage na kunirarua mifupa yangu yote kama simba katili anayerarua nyama
yangu, mimi ningali tumboni mwako. Nililia na kutoka machozi saa ile, nawe
ukaziba masikio yako. Nilikutazama kwa huzuni sana usoni, lakini ukanifumbia
macho mwanao.
Tumbo
lako lilipokuwa linakusokota, baada ya kuchomwa ile sindano, ni mimi niliyekuwa
nayeyuka, nanyumbuka viungo vyangu na kusononeka kwa uchungu sana Mama. Je,
Wewe leo kama mama yako asingekutetea ulipokuwa hujiwezi kama mimi leo ungekuwa
wapi mama? Je, ulimtendea jema gani mama yako tumboni mwake hata ukamfurahisha
asikuue? Kuniua mwanao niliyekupenda kwa moyo wangu wote! Kuniua mwana wa tumbo
lako mwenyewe! tena mwana wako mzaliwa wako wa kwanza? Mama mpenzi, huko ndiko
kunipenda kweli mtoto wako na kunitakia heri ya kweli kwa kunifungia hata
mlango wa Mbinguni, yaani bila hata kubatizwa, kweli mama yangu? Hebu fikiria
mama yangu unataka mimi niende wapi na
hata nifanye nini bila kuishi na Mungu? Ni kweli mama yangu hutaki hata
nimrudie Mungu wangu aliyeniumba kwa sura na mfano wake? Mama, Mama yangu!
kumbuka kuwa machozi yangu yanaanguka kifuani mwangu na kutiririka kifuani
mwako wewe mama yangu. Damu yangu Mama, kumbuka ni yako mwenyewe, uliyoamua
kuimwaga bure. Ule mwili wangu ulioutupa pale udongoni,ni mwili wenu ninyi
wazazi wangu uliotokana na ulevi wenu siku ile.
Mbali na kuwa nimekosewa haki zangu zote za kuishi
kama binadamu hapa duniani, bado kilio changu na damu yangu vinamlilia Mungu
wangu. Kama vile damu ya Abeli na wengine, ambao damu yao isiyo na hatia yoyote
ilimwagwa na bado inaendelea kumwagwa hapa dunia. Damu hizo zote bado
zinamlilia Mungu toka pale udongoni. Mungu wangu, ingawa wazazi wangu
wamenitupa, tafadhali sana nakuomba, Baba, wewe usinitupe milele. Mimi ni mtoto
wako, ingawa sistahili kuitwa hivyo. Baba pokea roho yangu uliyoiumba kwa sura
na mfano wako Mungu. Leo nairudisha roho yangu mikononi mwako Baba. Najua Mama
yangu ameniua mimi mwanae sababu ya ubinafsi wake, ili yeye aendelee na shule
na kujifurahisha na anasa za dunia hii. Na ndio maana hakujali kuniua mwanae mzaliwa wake wa kwanza
niliyempenda sana.
Haya,
kwaheri mama yangu! Tutaonana mbele ya safari panapo majaaliwa. Nawaombea
msamaha na Baba yangu Anton huko shuleni aliko.Nadhani naye sasa amejifunza
kitu, kwamba maisha ya kudanganyana yanamadhara. Naomba Mungu asilihesabu kosa
lao hili siku ya kiama.
Namaliza kwa kusema kuwa...
ASANTE MGANGA KWA KUTUMIA UTALAMU
WAKO KUUA WANYONGE. LAKINI SIKU YA KUPEWA KAZI HII SI ULIAPA KUWA KUUA KWAKO NI
MWIKO!?
ASANTE BABA KWA KUNILETA MWANAO
DUNIANI KWA MCHEZO TU NA ULEVI!.
ASANTE SANA MAMA YANGU, NI MIMI
MWANAO NAKUSALIMU, SHIKAMOO!KILA UKIPITA PALE KICHAKANI, DAIMA KUMBUKA KUWA
MIMI MWANAO BADO NIPO PALE ULIPONIFUKIA SIKU ILE!
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Simulizi hii iliwahi kutolewa
katika Gazeti la MWENGE mwaka 2013
Hivi punde simulizi hii itawekwa
kwa mtindo wa sauti ikirekodiwa kupitia Precious Records.
Ahsanteni
Baada ya kuwa na uhusiano naye kwa miaka saba, aliachana nami. Nilijaribu kila niwezalo kumrudisha lakini yote yalikuwa bure. Nilitamani arudi vibaya sana kutokana na mapenzi niliyonayo kwake na nilimsihi kwa moyo wangu wote, nilimpa ahadi lakini alikataa. Niliwasiliana na mganga aitwaye DR Dawn, ambaye angeweza kunisaidia kuniroga ili kumrejesha lakini mimi ni mtu ambaye sikuwahi kuamini uchawi, sikuwa na jinsi zaidi ya kujaribu. Nilimtumia barua pepe mganga huyo na akaniambia kwamba hakuna tatizo lolote, kwamba kila kitu kitakuwa sawa baada ya siku mbili na kwamba mpenzi wangu wa zamani angerudi kwangu baada ya siku tatu. Alipiga uchawi na cha kushangaza, siku ya pili, ilikuwa karibu 4:00 PM. Mpenzi wangu wa zamani alinipigia simu, tukasuluhisha tofauti zetu na sasa tuna furaha pamoja. Yeyote anayeweza kuhitaji usaidizi wa mtangazaji huyo anaweza kumtumia barua pepe kwa ( dawnacuna314@gmail.com ) au /WhatsApp kwa: +2349046229159
ReplyDeleteKwa uchawi wa kuungana tena.
Kwa ujanja wa ujauzito.
Kushinda bahati nasibu.
Kushinda kesi mahakamani.
Mimea ya kutibu, kila aina ya magonjwa kama,
VVU UKIMWI Kansa malengelenge na zaidi.